dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 28, 2017

Nay wa Mitego Apata Mwaliko Ikulu Kutoka Kwa Rais Magufuli!

Muda mfupi baada kuachiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam alikokuwa akishikiliwa kwa kosa la kutoa wimbo wa kuikashifu serikali, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Emanuel Elibariki (Nay wa Mitego), amealikwa Ikulu ya Dar es Salaam na Rais John Pombe Magufuli.
Akizungumza na kituo kimoja cha runinga, Nay alikiri kupata mwaliko huo na kueleza kwamba atakapokutana naye, ataitumia nafasi hiyo kumueleza mheshimiwa rais hali halisi ya maisha ya Watanzania.
“Nimepokea mwaliko bado nafikiria nini cha kuongea naye endapo nitapata hiyo nafasi ya kuzungumza naye, nadhani itakuwa nafasi nzuri ya kumweleza vile ambavyo Watanzania sisi tunaishi mtaani,”alisema.
Nay alikamatwa na polisi mkoani Morogoro usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa kile kilichodaiwa kutunga na kutoa wimbo wenye maudhui yanayoikashifu serikali.
Baadaya kukamatwa, Jumatatu ya Machi 27, 2017 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe alisema Rais Magufuli ameagiza msanii huyo aachiwe huru na wimbo wake uendelee kuchezwa na kusambazwa.
/GPL

No comments :

Post a Comment