Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, June 4, 2017

Lowassa: Rais Magufuli anafagia fedha za Watanzania!

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward Lowassa amefunguka na kusema kuwa Rais Magufuli alianza vizuri kwani yapo mambo aliyoyafanya ni mazuri lakini pia yapo mambo mengine amefanya yana matatizo.

Lowassa amesema haya alipokuwa akifanya mahojiano na kusema kwa sasa tumuache Rais Magufuli aendelee na kazi yake lakini baadaye ndiyo watu waweze kumuhukumu kutokana na mambo ambayo ameyafanya.

"Rais Magufuli ameanza vizuri kubana mambo mazuri amefanya lakini kuna mambo mengine yana matatizo, lakini Mwalimu Nyerere aliwahi kusema wakati unafagia, unaweza kufagia hata shilingi sasa Rais Magufuli anafagia shilingi nyingi. Lakini tumuachie aendelee na kazi tumuhukumu baada ya kipindi fulani" alisisitiza Lowassa.

No comments :

Post a Comment