dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, June 23, 2017

MASAUNI ASHIRIKISHA WADAU WA MAENDELEO KUENEZA HUDUMA YA MAJI KIKWAJUNI!

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto), akizungumza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa(UN)nchini, Alvaro Rodriges (kushoto), alipotembelea Mradi wa Maji Kikwajuni uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar,Dk. Ali Mohamed Shein miaka miwili iliyopita ikiwa ni juhudi za Mbunge huyo kushirikisha wadau katika kuhudumia na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa jimbo hilo. Kulia ni Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mhandisi Mohamed Elyas.na anayefuata ni Katibu wa taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Icon (TAYI), Abdallah Ahmed Suleiman Picha na Abubakari Akida
Katibu wa taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Icon (TAYI), Abdallah Ahmed Suleiman akimuonyesha Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN)nchini, Alvaro Rodriguez (wakwanza kushoto),ramani ya mpango wa uboreshaji huduma ya maji katika jimbo la Kikwajuni.Mratibu huyo amefika jimboni hapo ikiwa ni juhudi za Mbunge wa Jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto) katika juhudi zake za kutatua changamoto za huduma ya maji kwa wananchi.
Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mhandisi Mohamed Elyas, akitoa maelezo ya Mradi wa Maji Kikwajuni kwa Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodriguez alipotembelea mradi huo uliopo katika jimbo la Kikwajuni,Zanzibar.
Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN)nchini, Alvaro Rodrigues, akiangalia moja ya mabomba yanayotumika kusafirisha maji kwenda kwenye maeneo mbalimbali jimboni Kikwajuni ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na Mbunge wa Jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni() katika kuhakikisha anamaliza tatizo la upungufu wa maji jimboni hapo
Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN)nchini, Alvaro Rodrigues, akizungumza na Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar, Mhandisi Mohamed Elyas, wakati akiwasili kutembelea Mradi wa Maji wa Kikwajuni ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na Mbunge wa Jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni(katikati) katika kuhakikisha anamaliza tatizo la upungufu wa maji jimboni hapo
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Mkurugenzi Uzalishaji Maji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar(ZAWA), Mhandisi Mohamed Elyas(kulia) wakati wakiondoka baada ya kumuongoza Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN)nchini, Alvaro Rodriguez(kulia), kutembelea Mradi wa Maji wa Kikwajuni ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na wadau katika kuhakikisha anamaliza tatizo la upungufu wa maji jimboni.

No comments :

Post a Comment