Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, July 17, 2017

APANDISHA ‘MAPEPO’ NA KUWAUA WENZAKE WAWILI WAKIBATIZWA MTONI!

ROMBO: Waumini wawili wa Kanisa Siloam wamekufa maji wakibatizwa katika Mto Ungwasi wilayani Rombo baada ya mmoja wao kupandisha mapepo na kuwatumbukiza majini.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Agnes Hokororo amethibitisha tukio hilo lililotokea, Julai 16 saa sita mchana. Ubatizo huo ulifanyika kwenye kina kirefu cha mto huo. Amesema wakati ibada ya ubatizo mmoja wa waumini aliyepandisha mapepo alimtumbukiza mmoja wa watu waliokuwa wakisubiri kubatizwa na mchungaji.

Hokororo amesema muumini mmoja alipoona mwenzake ametumbukizwa majini aliamua kumwokoa, ndipo aliyepandisha pepo alipowashikilia wote wawili ndani ya maji na kuwasababishia kifo.

Amesema watu watatu akiwamo mchungaji wa kanisa hilo lililopo katika Kijiji cha Mandechini wanashikiliwa.


/ Mwananchi

No comments :

Post a Comment