dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, July 26, 2017

Hatimaye Jaribio la kifaa kinachowalinda wanawake dhidi ya HIV lafaulu!

Watafiti nchini Marekani wanasema kuwa jaribio ambalo vijana wa Marekani walitumia mpira wa mviringo kujilinda na virusi vya HIV limefanikiwa.

Utafiti zaidi sasa utafanyiwa vijana barani Afrika.

Wasichana walitumia mviringo wa plastiki uliowekwa dawa za kujilinda na ukimwi , ambao hulibadilishwa kila mwezi baada ya kipindi cha miezi sita.

Ni mojawapo ya mipango ya kutengeza kifaa ambacho wanawake watatumia kujilinda dhidi ya maambukizi ya HIV ili wasiweze kuwategemea wanaume kuvaa mipira ya kondomu.Wakiripoti ugunduzi huo mpya kuhusu virusi vya HIV mjini Paris, watafiti walisema kuwa wanafurahi kwamba wasichana hao walitumia mvirongo huo na kusema kuwa wameupenda.

Wanawake na wasichana walio na kati ya umri wa miaka 15-24 wanadaiwa kuwa moja kwa tano ya visa vyote vya maambukizi ya HIV duniani.

Takriban wanawake 1000 huambukizwa virusi kila siku katika Afrika ya jangwa la sahara.

No comments :

Post a Comment