dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, July 11, 2017

Kisiwa cha wanaume pekee Japan chatambuliwa na Unesco!

Kisiwa cha Okinoshima nchini Japan, ambapo wanawake hawaruhusiwi kufika, kimetambuliwa kama Turathi ya Ulimwengu na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, Unesco.

Kisiwa hicho cha Okinoshima huchukuliwa kuwa kitakatifu kiasi kwamba ni wanaume pekee wanaoruhusiwa kuzuru, gazeti la Asahi Shimbun linasema.

Na hata wanapofika huko, hawaruhusiwi kuondoka na chochote, hata kipande cha nyasi.Jopo maalum liliwasilisha pendekezo kwa Unesco watambue rasmi kisiwa hicho kama turathi ya ulimwengu mwezi Mei.

Katika kisiwa hicho, kuna madhabahu ya Munakata Taisha Okitsumiya, ambayo ni ya kumtukuza miungu wa baharini.

Katika kisiwa cha Okinoshima, kuliandaliwa matambiko kwa ajili ya usalama wa meli na pia wakazi wa Japan walitumia kisiwa hicho kuwasiliana na wakazi wa rasi ya Korea na China kati ya karne ya nne na tisa, gazeti la Japan Times linasema.

Bado kuna miiko kuhusu kisiwa hicho, mfano wanawake kupigwa marufuku.
Wageni wa kiume pia hutakiwa kwanza kuvua nguo zao zote na kufanya tambiko la kujitakasa.
Aidha, hawatakiwi kufichua chochote kuhusu waliyoshuhudiwa wakiwa kwenye kiswa hicho.

"Haya ni baadhi ya mambo ambayo itabidi yazingatiwe iwapo kitaorodheshwa kuwa turathi," anasema Asahi Shimbun, na kueleza kuwa huenda kisiwa hicho kikawa maarufu sana kwa utalii.
Zamani, hata kabla ya madhabahu kujengwa, kisiwa cha Okinoshima kilikuwa kikitumika kwa matambiko na mabaharia na pia kilihusika katika mashauriano ya kibiashara kati ya watu wa Korea na watu wa China.

Maelfu ya vitu vya kale, vilivyowekwa katika kisiwa hicho kama zawadi kutoka maeneo ya mbali, vimepatikana katika kisiwa hicho ikiwa ni pamoja na pete za dhahabu kutoka rasmi ya Korea, gazeti la Japan Times linasema.

Kisiwa hicho kwa sasa hupokea wageni siku moja pekee, 27 Mei, na sheria za kale bado hufuatwa.
Idadi ya wageni wanaoruhusiwa kufika kisiwa hicho kwa mwaka ni 200 pekee, Na lazima watimize matambiko yote baharini, na lazima wawe wanaume.

"Msimamo wetu kuhusu jinsia hautabadilika hata kama kitaorodheshwa kuwa Turathi ya Ulimwengu," afisa wa Munakata Taisha aliambia gazeti la Mainichi Daily, awali.

No comments :

Post a Comment