dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, July 24, 2017

Sakaya ana Damu ya CCM- JPM!

Rais John Magufuli amemmwagia sifa mbunge wa jimbo la Kaliua - Tabora (CUF) Magdalena Sakaya kwa kupigania maendeleo ya wananchi na kusema kuwa, mwili na tabia yake ni za CUF lakini roho na damu yake ni ya CCM.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Julai 23 wakati wa ziara yake mkoani Tabora na kuwataka wabunge wa CCM kumpa ushirikiano anapofanya shughuli za maendeleo.
“Nimpongeze mbunge wa jimbo hili. Ingawa mwili na maneno na tabia zake ni CUF, lakini roho yake na damu ni CCM. Inawezakana hata siku zijazo akahamia CCM. Anajitahidi kuleta maendeleo ingawa hayachagui chama  ” amesema.Aidha Dkt. Magufuli ameongeza kuwa "Ni mara 10 uwe na CUF, Chadema au NCCR anayefanya mambo ya CCM kuliko uwe na CCM anayefanya mambo ya vyama vingine. Hasara yake ni kubwa mno, mnafikiri ni mwenzenu wakati siyo mwenzenu, nani hayajui haya hata wakati wa kampeni yalitokea unafikiri siyajui,” amesema.

Pamoja na hayo amewataka wabunge wa CCM kumpatia ushirikiano mbunge huyo na kuwataka wasimbague kama yeye jinsi asivyowabagua.

No comments :

Post a Comment