dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, July 17, 2017

Tajirika kwa kuanzisha kampuni ya kuuza umeme wa solar panel!

Kuna upungufu mkubwa umeme wa uhakika kutoka katika makampuni yanayotoa hudumu hiyo katika Africa kuna wastani wa siku si chini ya 300 wa jua kuonekana kwa uwazi bila mawingu licha ya hiyo solar panel zinahisi tu mwanga na kuhifadhi umeme kwa sababu hiyo umeme wa solar ni wauhakika, rahisi, na gharama ndogo. Africa wako na nafasi nzuri ya kuendeleza umeme wa jua.

Mfano mzuri ni Jasper Power Plant ya South Africa ambayo ilianza na mtaji mdogo lakini kwa sasa ina billion ya dola kwa kuzalisha 100Megawatts na kutoa huduma ya kuuza umeme zaidi ya nyumba 30,000.Gharama za umeme kutika mashirika ya umma zimekuwa zikipanda kila kukicha kwanini usijiajiri na kuuza umeme wa uhakika wa solar angalua kwa nyumba tano tu hapo mtaani kwako.Na uone jinsi uhitaji ulizo mkubwa.Biashara ya solar imefanya baadhi ya watanzania kuwa mabilionea wakubwa mfano mzuri ni Patrick Ngowi mwazilishi wa Helvetic Solar miaka kumi iliyopita akiwa na miaka 19 alipokea mkopo kutoka mama yake wa kuanzisha biashara.Alianza kwa kuuza simu za kichina na akagundua uhitaji mkubwa wa umeme kwa ajili ya simu anazouza.Wakati wa safari zake china akanunua solar ndogo na vifaa vyake.

Mda mfupi tuu mwaka 2013 akaanzisha kampuni yake ya Helvetic Solar Contractrs mwaka huo huo ikaingiza zaidi ya dola 5million(10billionTsh).Wala Patrick hakuwa na mtaji mkubwa sana!! wala hakuwa na mwekezaji!!! wala hakuwa na msaada wa serikali!!! hata ujuzi hakuwa nao.Leo Patrick Ngowi ni tajiri mkubwa sana chini ya miaka 30.

No comments :

Post a Comment