dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 20, 2017

Mambo 4 Makubwa aliyofanya Rais Shein leo Zanzibar!


Rais wa serikali ya mapinduzi na mwenyekiti wa baraza la wawakilishi Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein ameanza ziara ya siku tatu leo hii katika mkoa wa Mjini Magharibi ambayo inagusia zaidi ukaguzi wa miradi ya maendeleo, uzinduzi miradi iliyokamilika sambamba na usikilizwaji wa kero za Wananchi na kuzipatia majibu.

1. Ikiwa ni siku ya kwanza ya Ziara hiyo, Mheshimiwa alianza kwa kukagua shughuli za ujenzi wa kiwanja cha mpira cha Mao Zedong kilichopo Kiwajuni Unguja, Mkoa wa mjini wa magharibi, na Hapo alilkuwa akipokea taarifa za ujenzi huo kutoka kwa Injinia Hassani Omary Hassan.

2. Rais Shein amekagua mradi wa kuzuia kasi ya mawimbi ya bahari katika eneo la kilimani- Kizingo, ambapo Meneja mradi huo Bernad Oldonyo amemueleza Rais Shein mradi huo unaendelea vuzuri na kwamba utakamilia katika muda mfupi ujao.


3. Rais Shein ameweka jiwe la msingi katika chuo cha utalii kilichopo Maruhubi Mkoani Mjini Magharibi ambapo Kwamujibu wa Mkandarasi wa mradi huo Yusuph Mlimakifi amemueleza Rais Shein kuwa ujenzi huo umefikia asilimia hamsini.

4. Katika sehemu ya mwisho ya ziara hiyo kwa leo Ijumamosi 19/ 08/ 2017, Rais Shein ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amezindua tawi la CCM la Matarumbeta ambapo amewataka viongozi wa chama kuhakikisha wanawatumikia wananchi kama ilivyoelekezwa kwenye ilani ya chama cha mapinduzi.
Rais Shein ataendelea na ziara kesho Siku ya Ijumapili katika wilaya ya Mjini magharibi 'A' na siku ya Ijumatatu atamalizia katika wilaya ya Magharibi 'B'


Ziara hiyo ni ya kwanza kwa Rais Shein tangu achaguliwe katika uchaguzi wa marudio mwaka jana, Na ni ya tatu tangu aingie madarakani mwaka 2010.

No comments :

Post a Comment