dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 3, 2017

UN yatoa ripoti ya hali mbaya ya kisiasa Burundi!

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea kusikitishwa na hali mbaya ya kisiasa nchini Burundi zikiwemo taarifa za ongezeko la idadi ya wakimbizi na taarifa za mateso, kulazimishwa kupotea na mauaji ya kinyama.

Katika ripoti hiyo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limesema limekusudia kuchukua hatua kwa wote wanaohusika na matukio hayo ndani na nje ya nchi hiyo ambapo limesema linatishia amani na usalama wa Burundi.

Katika taarifa yake Baraza hilo la Usalama limeitaka serikali ya Burundi na pande zote zinazohusika kuacha mara moja na kukataa matukio hayo ya vurugu.Katika taarifa hiyo iliyosomwa na Balozi Amr Abdellatif Aboulatta wa Misri ambaye ndio mwenyekiti wa Baraza hilo, amesema baraza hilo linasikitishwa na hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea Burundi ambapo zaidi ya wakimbizi laki mbili wamekuwa wa ndani, huku watu raia milioni tatu wakiwa na mahitaji na zaidi ya raia laki nne wakitafuta ukimbizi katika nchi za jirani.

Baraza hilo limeshukuru nchi zinazopokea wakimbizi kwa jitihada zao, mataifa ya kikanda kwa kuheshimu wajibu wao wa kimataifa hasa katika kujali hadhi za wakimbizi na kuhakikisha wanarejea waliokotoka kwa hiari yao kwa kuzingatia uamuzi wao na taarifa za usalama na utu wa binadamu.

Kwa upande mwingine Baraza hilo limelaani vikali matamko katika umma ambayo yamekuwa yakihamasisha vurugu na chuki dhidi ya raia ikiwemo wito wa kulazimisha kuwapa ujauzito wanawake na wasichana na kuitaka serikali na pande zote kusitisha mara moja vurugu na kulaani kauli zote za chuki.

No comments :

Post a Comment