Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, September 18, 2017

BAVICHA Watangaza siku rasmi watakayosoma Albadili!


Baraza la Vijana wa CHADEMA wilayani Muheza mkoani Tanga wamekanusha kusoma albadili ambayo walidhamiria kuifanya siku chache zilizopita, wakisema bado wanalipa muda huku mtaani kukiwa na tetesi kuwa ilishasomwa.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television mwenyekiti wa BAVICHA Muheza, Joseph Saja, amesema sababu ya zoezi hilo kutofanyika ni kwamba siku walizotangaza kuwataka waliofanya tukio hilo kujisalimisha zilikuwa hazijaisha, hivyo wataendelea na zoezi hilo mapema wiki ijayo.
"Siku ambazo tuliwapa wale watu kujitokeza ilikuwa mwisho Ijumaa, na mpaka leo bado hawajajitokeza sasa ndio tutatekeleza majukumu yetu ya kuanza kwenda huko tunakoenda kuisoma, inawezakana katika juma tatu au jumanne ndio tutatoka kwenda", amesema Joseph Saja.

Wiki iliyopita BAVICHA wilayani Muheza mkoani Tanga walitangaza kusoma albadili ili kuwajua watu waliomshambulia kwa risasi Tundu Lissu, na kuisaidia serikali ambayo mpaka sasa haijafahamu waliohusika.

No comments :

Post a Comment