Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 19, 2017

Mbunge Ibrahim Raza, mgeni rasmi sherehe ya mahafali ya kwanza ya kidati cha nne skule ya Kiembe Samaki “A” Islamic!

Mwanafunzi Suleiman Hafidh alieigiza kama Daktari akiongoza wenzake kwenye onesho la kufanya upasuaji wakati wa Mahafali ya kwanza ya kidato cha nne Skuli ya Sekondari Kiembe Samaki “A” Islamic, yaliyofanyika skulini habo Mazizini Mjini Unguja.
Mwanafunzi Mathna Tahir akisoma risala ya wanafunzi katika Mahafali ya kwanza yakidato cha nne ya Skuli ya Sekondari Kiembe Samaki “A” Islamic.
Msaidizi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari Kiembesamaki “A” Islamic Mohammed Shaib Same, akielezea mikakati yao katika kuboresha elimu kwa mgeni rasmi Mbunge wa jimbo la Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza, alipohudhuria mahafali ya kwanza ya skuli hiyo.
Mhe. Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Raza akiwahutubia wazazi na wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kiembesamaki “A” Islamic katika mahafali ya kwanza ya skuli hiyo yaliyofanyika Mazizini Mjini Unguja.
Wanafunzi na wazazi waliohudhuria mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya Skuli ya Sekondari Kiembe Samaki “A” Islamic wakifuatilia hutuba ya Mbunge wa Kiembesamaki Ibrahim Raza.
Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Raza akimpa cheti mwanafunzi Mamissa Maalim aliyefanya vizuri zaidi kwenye somo la hesabati.
Mhe. Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Raza (katikati) katika picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo yao. Kulia waliokaa ni msaidizi Mwalimu Mkuu Skuli Sekondari Kiembesamaki “A” Islamic Mohammed Shaib.
Muonekano wa Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki “A” Islamic iliyopo Mazizini Mjini Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga.

No comments :

Post a Comment