Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 14, 2017

Atiwa nguvuni baada ya kutaka kuwauza watoto wake mapacha!

Mwaka 2013 wasichana wajawazito 17 na watoto 11 waliokolewa wakati polisi walivamia "kiwanda cha watoto" katika jimbo la Imo.
Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya madai kuwa alijaribu kuwauza watoto wake pacha wenye umri wa mwezi mmoja nchini Nigeria.

Ameshtaki kwa kuhusika katika bishara ya kuuza watoto lakini polisi wanasema kuwa mashtaka zaidi yataongezwa.

Mwanamke huyo alikamatwa wakati akijaribu kuuza watoto wake wasichana kwa dola 980 kwa mnunuzi ambaye aliwajulisha polisi.

Visa vya kuuzwa watoto wa kupangwa vimekuwa tatizo kwa muda mrefu chini Nigeria.

Nigeria ni mzalishaji mkuwa wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu milioni 170 wanaishi kwenye umaskini.
Alipohojiwa mwanamke huyo alisema kuwa changamoto za kifedha zilisababisha afanye hivyo.

Mwaka 2013 wasichana wajawazito 17 na watoto 11 waliokolewa wakati polisi walivamia "kiwanda cha watoto" katika jimbo la Imo

Miaka miwili baada ya sakata hilo, mwanamke mwingine alishikwa alipokuwa akijaribu kumuuza mtoto wake kwa dola 90 katika jimbo la Cross River.

No comments :

Post a Comment