Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 10, 2017

Bei ya Korosho yatakata, wakulima Liwale, Ruangwa na Nachingwea kicheko kinene!

BEI ya korosho katika mnada wa nane kwa chama kikuu cha cha ushirika cha RUNALI uliofanyika leo katika kijiji cha Mikunya wilaya ya Liwale imeongezeka ikilinganishwa na bei ya juma lililopita.Kwamujibu wa ofisa wa idara ya maendeleo na ushirikina toka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, Robert Nsunza katika mnada huo barua 37  za waombaji ununuzi wa zao hilo zilisomwa.

Nsunza alisema katika ghala la Lindi farmers lililopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Nachingwea barua 19 ziliomba kununua korosho zilizopo katika ghala hilo. Huku barua 18 zikiomba kununua katika ghala la umoja lililopo mjini Liwale.

Ofisa huyo alizitaja kampuni zilizoshinda zabuni kuwa ni San Shain, iliyonunua tani 1000 zilizopo katika ghala la Lindi farmers kwa bei ya shilingi 3,935, kampuni ya RCC tani 400 zilizopo katika katika ghala hilo la Lindi farmers, kwa bei ya shilingi 3,932.

Alizitaja kampuni nyingine kuwa ni Iscon commodity na Kasuga General trade. Ambazo zimenunua katika ghala la umoja. Ambapo Iscon imenunua tani 400 kwa bei ya shilingi  3875 kwa kila kilo moja. ambapo kampuni ya Kasuga imenunua tani 300 kwa shilingi 3873 kwa kila kilo moja.

"Bei hizo ni tofauti na zile za juma lililopita, kwani bei ya juu ilikuwa shilingi 3860, na bei ya chini ilikuwa shilingi 3733. Hivyo bei imeongezeka, alisema Nsunza.

Akizungumza katika mnada huo, mwenyekiti wa RUNNALI, Hassan Mpako alitoa wito kwa wakulima walioazima magunia katika vyama vyao vya msingi nakiendelea kubaki nayo katika majumba yao wazirejeshe haraka.

Alisema miongoni mwa sababu zilizochangia korosho nyingi kushindwa kuondolewa kwenye maghala ya vyama vya msingi ni upungufu wa magunia. Hivyo kusababisha mrundikano na kuchelewa kuuzwa korosho hizo.

Alisema kwakuwa baadhi ya wakulima hawataki kurejesha magunia kwa hiari, inabidi waanzishe msako.

"Viongozi wa vyama vya msingi kuweni na takwimu sahihi za watu waliochukua magunia, sisi tutadili na nyinyi. Magunia yale sio ya kuhifadhia korosho majumbani mwao. Lakini sasa wanadabanisha korosho kushindwa kupelekwa kwenye maghala mkuu na kusababisha malalamiko, "alionya Mpako.

Kwa upande wake meneja mkuu wa chama hicho, Christopher Mwaya, alisema hadi sasa malipo ya wakulima ya minada sita kati ya nane fedha zake zimeingizwa kwenye akaunti za vyama Vya msingi. Huku akibainisha kuwa malipo ya mnada wa saba yanaandaliwa.

Katika mnada huo kampuni 30 zilijitokeza kuomba kununua. Hiyo ni tofauti na mnada wa wiki iliyopita. Ambapo kampuni zilizojitokeza zilikuwa 22 tu.

No comments :

Post a Comment