Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amefunguka na kusema wao CCM hawajawahi kuzungumzia juu ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kushikilia nafasi hiyo kwa muda mrefu bila kufanya mabadiliko.Polepole amesema hayo wakati akimjibu moja ya mwananchi ambaye alitaka kufahamu kuwa ni kwanini Wanachama wa CCM wao ndiyo wamekuwa wakipiga sana kelele juu ya nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, ndipo hapo alipofunguka na kusema hawajawahi kuzungumzia hilo na kwa kuwa hakuna mwengine ambaye wanaona anafaa basi aendelee Mbowe kwa miaka 100.
"Msemaji wa CCM ni mimi na hatujawahi kutoa kauli hiyo, huyo Mwenyekiti maadamu hakuna mwingine anayefaa kuliko yeye aendelee tu miaka 100" aliandika Polepole
Mbali na hilo Polepole ameulalamikia upinzani wa Tanzania kwa sasa na kusema umekuwa wa kupinga kila kitu hata kwa mambo mazuri wenyewe umekuwa ukipinga tu hivyo amefananisha kuwa huenda hiyo ni siasa mpya.
"Upinzani wa bongo mtihani, useme wewe nikisema mimi itakuwa shida, kila zuri siku hizi litapingwa naona ni siasa mpya" alisema Polepole.

No comments :
Post a Comment