Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 31, 2017

Kigwangalla: kakobe ana Ugonjwa wa Akili!

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa ukimpeleka mahakamani Askofu Zacharia Kakobe atashinda kwasababu watu wanasema inawezekana anasumbuliwa na ugonjwa wa akili.Kigwangalla ameyasema hayo leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ambapo ameeleza kuwa ugonjwa unaotajwa kuwa huenda unamsumbua Kakobe dalili zake ni kujisifia.

Kigwangalla amefafanua aina ya ugonjwa huo wa akili ambao inawezekana unamsumbua Askofu Kakobe kuwa ni 'Bipolar Disorder: Currently Mania’. Pia amesisitiza kuwa hata ukimpeleka mahakamani anaweza akashinda kwa kigezo hicho.

''Kuhangaika na mtu kama KAKOBE  ni kupoteza muda bure. Kuna watu wanasema inawezekana akawa na ugonjwa wa akili ‘Bipolar Disorder: Currently Mania’ ambao katika dalili zake ni ‘delusions of grandeur’ . Akipelekwa mahakamani anaweza kutetewa kwa kigezo hiki na akashinda!'' ameandika Kigwangalla.

No comments :

Post a Comment