dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 10, 2017

Kisa Babu Seya mashabiki wamvaa Zitto!

Rais John Magufuli amevunja rekodi kwqa kusamehe wafungwa 8,157 ikiwamo familia ya mwanamuziki wa dansi Nguza Vicking ‘Babu Seya’  na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ jana Jumamosi.Rais Magufuli alitangaza uamuzi huo wakati akihutubia maadhimisho ya sherehe ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika mjini Dodoma.

Hata hivyo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuonyesha kutokubaliana na uamuzi huo kwa madai  kwamba  anashaangaa kuachiwa watu waliohukumiwa kwa sheria ya nchi.

Posti hiyo ya zito ilizua mjadala mtandaoni kutokana na watu mbalimbali kumshukia kwa kuonyesha kukerwa na alichokiandika. Baadhi ya wasomaji walimsihi kuachana na jambo hilo kwani Rais ametimiza wajibu wake kisheria.

No comments :

Post a Comment