Wakazi wa mji wa Dodoma na viunga vyake mapema leo Jumamosi, Desemba 9, 2017 wamejitokeza kushuhudia maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Taratibu za ukaguzi wa kiusalama, zilifanya misururu mirefu baada ya kutumika geti moja kuingilia ndani ya Uwanja wa Jamuhuri.
Hali hiyo ilifanya misururu mrefu kuanzia geti la kuingilia uwanjani kufika katika barabara inayoelekea Nkuhungu.
Mabasi makubwa yanayotoka katika wilaya za jirani yalionekana yakishusha watu tangu saa 11.00 alfajiri kuwahi foleni.Watu walianza kuingia uwanjani huku vikundi mbalimbali vya burudani vikitumbuiza.
Saa 2:00 asubuhi, gwaride maalumu lililojumuisha vikosi vya ulinzi na usalama viliingia uwanjani.
Viongozi mbalimbali walianza kuwasili uwanjani kuanzia saa 1:00 asubuhi wakiwemo mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mama Fatma Karume, mke wa Rais ya Kwanza wa Tanzania Mama Maria Nyerere na aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais, Mohammed Gharib Bilal.
Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema ni baadhi ya viongozi wa kisiasa walioonekana uwanjani hapo.
Viongozi wengine waliofika asubuhi uwanjani hapo ni Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, mke wa Rais, Janeth Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, majaji wakuu wa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, Spika wa Bunge Job Ndugai, mawaziri na wabunge.
Tayari Uwanja wa Jamhuri umejaa na wananchi wamezuiwa kuingia katika uwanja huo na milango yote imefungwa.

No comments :
Post a Comment