Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. John Magufuli kuwafuatilia mahabusu waliokaa magereza muda mrefu bila kesi zao kukamilika.Mh. Lema amefunguka hayo kwenye ukurasa wake Twitter ambapo amechukua hatua hiyo baada ya kumshukuru rais Magufuli kwa kitendo cha kutoa msamaha kwa watu 8157.... waliokuwa wamehukumiwa katika magereza tofauti nchini.
"Mh Rais Magufuli, Mungu akubariki sana kwa msamaha uliotoa jana kwa wafungwa haswa wale waliokaa magereza muda mrefu pamoja na wazee, msamaha ni ibada, pia wako mahabusu wamekuwa magereza kwa muda mrefu sana bila kesi zao kukamilika. Mh Rais fuatilia watu kama hawa pia" Lema.
Jana katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa miaka 56 ya Tanganyika yaliyofanyika Mkoani Dodoma Rais Magufuli alitangaza msamaha kwa wafungwa 8,157. ambapo baada ya msamaha huo, 1828 watatakiwa kuondoka Magereza kabisa na wengine 6329 wamepunguziwa muda wa kukaa gerezani.

No comments :
Post a Comment