zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 28, 2018

Afghanistan yaituhumu Pakistan kwa kuwaunga mkono wapiganaji!


Utawala nchini Afghanistan, umeituhumu Pakistan kwa kuwaunga mkono wanamgambo ambao walisababisha vifo vya zaidi ya watu 95 katika mlipuko wa bomu wa kujitoa mhanga mjini Kabul.

Watu 158 wamejeruhiwa.

Unasema kwamba, shambulio hilo la jana Jumamosi, lililotekelezwa na kundi moja la wapiganaji la Haqqani, lililo na uhusiano mkubwa na lile la Taliban, na kuungwa mkono na Pakistan.Utawala wa Afghanistan, sasa unaeleza kuwa shambulio hilo ni la kiwango cha mauwaji makubwa ya halaiki, dhidi ya binadamu.

Siku zote Islamabad imekanusha madai ya aina yoyote ya kuyaunga mkono makundi ya wanamgambo yenye nia ya kuhujumu utawala wa Afghanistan.


Marekani kuongeza askari Afghanistan

30 wafariki katika mlipuko Afghanistan

Taliban wawaua wanajeshi 26 wa Afghanistan


Gari moja la dharura la kuwahudumia wagonjwa, ambalo lilikuwa limejazwa vilipuzi, lililipuka katika kituo cha usalama barabarani baada ya kusimamishwa na askari, katika Wilaya ya Jiji Kuu Kabuli kulikokuwa na idadi kubwa ya watu.



Kwa njia ya taarifa, Rais wa Marekani Donald Trump, amelaani shambulio hilo, huku akitoa wito wa mbinu muafaka wa kupambana na kundi la Taliban.

Shambulio la sasa limetokea wiki moja tu baada ya Hoteli ya Intercontinental mjini Kabul kushambuliwa na watu zaidi ya 20 wakauwawa.

1 comment :

  1. prothom alo is the best bangla news site . if you more bangla news to visit this site.prothom alo

    ReplyDelete