zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 28, 2018

Lissu aelezea mambo aliyoyafanya katika urais wake wa TLS!

Shambulio la risasi dhidi ya Tundu Lissu limesababisha rais huyo wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), atumikie nafasi hiyo kwa miezi sita baada ya kujeruhiwa vibaya.Lissu, ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Ubelgiji kwa ajili ya awamu ya mwisho ya matibabu yanayohusisha mazoezi, alichaguliwa kushika nafasi hiyo Machi 18 mwaka jana.

Lakini alitumikia nafasi hiyo hadi Septemba 7 aliposhambuliwa na risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana akiwa nje ya makazi yake mjini Dodoma baada ya kutoka bungeni.

Baada ya shambulio hilo, alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na usiku wa siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi ambako alilazwa hadi Januari 6 alipohamishiwa Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

Chama hicho cha mawakili hufanya uchaguzi wa rais wake kila mwaka, hivyo uchaguzi wa mwaka huu utafanyika Aprili, jambo ambalo Lissu amelieleza gazeti la Mwananchi kuwa angetamani awepo kushiriki kama ilivyokuwa mwaka jana.

Akizungumza kuhusu nafasi yake hiyo ndani ya TLS, Lissu alisema: “Urais wangu wa TLS unafikia kikomo Aprili mwaka huu. Nataka niwepo siku hiyo, niwaeleze katika kipindi changu cha mwaka mmoja yapi tumefanya, lakini bado mimi ni mgonjwa.

“Lakini niwashukuru sana TLS walionichangia fedha za matibabu. Si TLS pekee hata taasisi na watu binafsi, wamewazidi hata Bunge ambalo limekwepa wajibu wake wa kisheria wa kunigharimia matibabu. Nawashukuru sana wale wanaoendelea kujitoa kwangu.”

Akizungumzia kutokuwapo kwa Lissu katika majukumu yake ya kiofisi, makamu wa rais wa TLS, Godwin Ngwilimi alisema tangu walipochaguliwa hadi sasa wamefanikiwa kufanya mambo kadhaa, kama kujenga jengo la kitega uchumi na kupunguza ada zilizokuwa zikilalamikiwa na wanachama.

Alisema wanakamilisha mfumo wa mafunzo kwa wanachama, yatakayomuwezesha wakili kupata mafunzo ya ubobezi katika eneo moja, kuweka uhuru wa wanachama kujiunga na vyama vingine vya kitaaluma.

“TLS si Lissu. TLS ya sasa tumeijenga kuwa taasisi isiyotegemea mtu mmoja. Tunataka ijiendeshe, iwatumikie wanachama wake ipasavyo,” alisema.

“Na hata ripoti zake ziwe zinatoka kwa wakati, tumefanya mengi ndani ya kipindi chetu mpaka sasa.”

Katika uchaguzi wa Machi 18 mwaka jana, wajumbe wa mkutano mkuu wa mawakili uliofanyika jijini Arusha walimpa Lissu asilimia 88 ya kura zote baada ya kupata kura 1,411 kati ya 1,682.

Wengine waliokuwa wakigombea nafasi hiyo ya urais ni Victoria Mandari, Francis Stolla, Godwin Mwapongo na Laurence Masha, ambaye hata hivyo, alijitoa dakika za mwisho kisha kutangaza kumuunga mkono Lissu.

Kabla ya uchaguzi uliopita wa TLS, Lissu alikumbana na vikwazo ikiwa ni pamoja na onyo la Serikali kukitaka chama hicho kutoingiliwa na siasa.

Dk Harrison Mwakyembe, ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, pia aliwatahadharisha viongozi wa TLS kutojihusisha na siasa, huku baadhi ya wanasheria akiwamo Godfrey Wasonga wakifungua kesi kumpinga Lissu kugombea nafasi hiyo. Hata hivyo, Lissu alishinda kesi hiyo.

Siku moja kabla ya uchaguzi wa TLS uliofanyika jijini Arusha, Lissu alishikiliwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Baada ya kusomewa mashtaka, alijidhamini na kwenda Arusha kushiriki uchaguzi na kuibuka na ushindi huo.


 / Mwananchi.

No comments :

Post a Comment