AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, February 27, 2018

Rais Ramaphosa atangaza baraza la Mawaziri Jipya!

Rais Cyril Ramaphosa Jumatatu ametangaza Baraza la Mawaziri jipya mabadiliko yaliyotarajiwa tangu alipoteuliwa na kuapishwa kushika wadhifa huo aliochukua baada ya mtangulizi wake, Jacob Zuma kujiuzulu.

Ramaphosa alisema mabadiliko hayo "yanalenga kuhakikisha kwamba Serikali ya kitaifa imejipanga vizuri kutekeleza majukumu yake ya utawala ".

Katika baraza hilo alilolitangaza siku 11 tangu alipoingia ofini linamjumuisha Nhlanhla Nene, ambaye alifutwa kazi na Jacob Zuma kama waziri wa fedha.

Ramaphosa aliweka msimamo wake kwa kumteua Nene wakati akishangaza kwa kumteua David Mabuza, waziri mkuu wa sasa wa jimbo la Mpumalanga kuwa naibu rais.

Ramaphosa alitangaza jumla ya mabadiliko 30 ya mawaziri na nafasi ya naibu baada ya Zuma kushinikizwa  kujiuzulu na chama cha chama cha chama cha ANC mapema mwezi huu.

"Katika mabadiliko hayo, nimetilia maanani zaidi haja ya kusawazisha uendelevu na utulivu na haja ya kuweka sura mpya, kufufua uchumi na kuchepusha kasi ya marekebisho," alisema Ramaphosa alipokuwa akisoma taarifa fupi kupitia televisheni.

Washirika wengi wa Zuma waliachwa au kufutwa kazi, lakini mke wa zamani wa Zuma, Nkosazana Dlamini-Zuma alichaguliwa kuwa waziri wa nchi katika ofisi ya rais anayehusika na mipango, ufuatiliaji na tathmini.

Ramaphosa alimshinda Dlamini-Zuma katika mchuano mkali wa kuchaguliwa kiongozi mpya wa ANC mwezi Desemba.

Mwanasiasa mwingine aliyerejeshwa kwenye baraza ni Pravin Gordhan ambaye anakuwa waziri wa biashara. Kuondolewa kwa Gordhan kutoka wizara ya fedha katika mabadiliko ya mwaka jana kulizusha maandamano na hofu kubwa.

No comments :

Post a Comment