Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, March 16, 2018

Kikwete ajitokeza na kulisifu Jeshi la Polisi!

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka na kulipongeza jeshi la polisi Tanzania kwa kuweza kufanikisha kukamatwa kwa watu ambao walikuwa wakitumia vibaya majina yake, mkewe na mtoto wake kuwaibia watanzania.Yakiwa yamepita masaa kadhaaa toka Jeshi la Polisi nchina Tanzania litangaze kuwakamata wanawake watatu ambao walikuwa wakitumia majina ya Rais mstaafu na mkewe kwa kuiba fedha za wananchi kwa kuwalaghai kuwa wanatoa mikopo kupitia Vicoba kwa njia ya mtandao wa facebook, Kikwete aibuka na kumpongeza IGP Sirro.

"Natoa pongezi nyingi kwa IGP Simon Sirro na Polisi Tanzania kwa kuwakamata watu waliokuwa wanatumia vibaya jina langu, la mke wangu Salma na mwanetu Ridhiwani kuwahadaa na kuwaibia Watanzania ninaowapenda sana. Kubainika kwa mtandao huo na kukamatwa ni hatua nzuri ya kupongezwa" alisema Jakaya Kikwete

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa watu hao ambao wamekamatwa na jeshi hilo la polisi watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

No comments :

Post a Comment