zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, March 30, 2018

SHULE YAVAMIWA NA MASHETANI..DC AZUNGUMZIA WAZEE KUITA WAGANGA KUTOKA KONGO!



Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mohamed Mtanda ametolea ufafanuzi suala la shule ya Msingi Kabwe kuita waganga wa kienyeji kutoka Kongo, ili kutatua tatizo la kishirikina linaloikabili shule hiyo ambapo inadaiwa shule hiyo imevamiwa na mashetani na kusababisha wanafunzi kuanguka ovyo,kupiga kelele na kuzimia.
 Mkuu wa Wilaya hiyo Said Mtanda amesema kwamba ni kweli alipokea simu kutoka kwa Mkuu wa shule hiyo kumuelezea matatizo yao hapo shuleni, na lengo walilofikia serikali ya kijiji ili kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara.

Licha ya hayo mkuu wa wilaya hiyo amesema yeye kama kiongozi wa serikali ni kulichukua tatizo hilo kitaalamu kwa kupeleka madaktari ambao watatafuta njia sahihi ya kutibu wanafunzi hao, na sio kuruhusu mambo ya kishirikina, ingawa hawezi kuwakataza wazee wa kijiji hicho kwani anaheshimu mila zao.

“Nilipokea simu kutoka kwa mkuu wa shule hiyo akinielezea matatizo yao, akaniambia na uamuzi wa kijiji ulivyoamua, lakini mimi kama kiongozi wa serikali nitawajibika vile ipasavyo, nitapeleka mganga mkuu wa wilaya akaangalie na namna ya kuweza kulimaliza tatizo hilo, ni tatizo ambalo mara nyingi hujitokeza mara nyingi kwenye shule zetu, lakini wao kama wanakijiji na wazee na ndio wazazi, wana uamuzi wao ambao siwezi kuwakataza, suala la kuita waganga kutoka Kongo sio kweli isipokuwa wana mpango wa kufanya matambiko yao, hayo ya waganga wa Kongo halipo”, amesema Saidi Mtanda.

Wanafunzi wa kike wa shule ya msingi Kabwe iliyopo Wilayani Nkasi mkoani Rukwa wanakabiliwa na tatizo la kiafya la kuanguka, kuzimia na kupiga kelele, jambo ambalo wakazi wa eneo hilo wanahisi linatokana na ushirikina, na kuamua kutafuta waganga wa kienyeji kuweza kutatua.

No comments :

Post a Comment