Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa kongamono la kumbukumbu ya hayati sheikh abeid amani karume lililoandaliwa na chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere kampasi ya zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa kongamono la kumbukumbu ya hayati sheikh abeid amani karume lililoandaliwa na chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere kampasi ya zanzibar.
Mkuu wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein wakati alipowasili kwenye kongamano la kumbukumbu ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Mark Mwandosya akiongea wakati wa kongamano hilo.
Waziri wa Vijana,Sanaa, Utamaduni na Michezo Balozi Ali Karume akizungumza wakati wa kongamano hilo.waliokaa ni watoa mada Balozi Amina Salum Ali na Mohamed Seif Khatib.
Mwenyekiti wa kongamano Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho akiongoza majadiliano wakati wa kongamano hilo.
Mgeni rasmi katika kongamano Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na meza kuu pamoja na wajumbe wa bodi ya chuo.

Mgeni rasmi katika kongamano Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na meza kuu pamoja na Wanafunzi wa skuli za msingi na sekondari waliofanya vizuri katika uandishi wa insha juu ya mchango wa Sheikh Abeid Amani Karume katika maendeleo ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amewaasa vijana wa Zanzibar kuwa Wazalendo na nchi yao kwa kuisoma na kuijua historia ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuenzi mchango wa Mwasisi wa Taifa hilo Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Dkt. Shein ameyasema hayo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi katika kongamano la kwanza la kumbukumbu ya Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, lililofanyika katika Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika kampasi ya Zanzibar, iliyopo Bububu mjini Magharibi siku ya Alhamis tarehe 5 April, 2018.
“Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, alikuwa ni mtu mvumilivu na mstahimilivu, aliyeipenda Zanzibar na wananchi wake, hivyo ni vyema mchango wake katika kuleta maendeleo ya Zanzibar ukakumbukwa na kuenziwa.
Rais Karume ametumia fursa hiyo pia kukipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuona umuhimu wa kuandaa Kongamano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika visiwani Zanzibar”
“Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imeandaa Kongamano hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya kuwaenzi waasisi wa Taifa ambao ni Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume ambao wanamchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa” amesema Rais Shein.
Katika taarifa yake, Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof.Shadrack Mwakalilia alieleza kuwa Hayati sheikh Abeid Amani Karume alipigania mengi kwaajili ya ustawi wa Zanzibar, na ndio sababu Chuo kikaona umuhimu wa kuandaa kongamano hilo kwa lengo la kujikumbusha na kujadili falsafa na ndoto za Sheikh Abeid Amani Karume katika ustawi wa Zanzibar ya leo.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Prof.Mark Mwandosya alimuahidi Dkt. Shein kuwa Chuo kitaendeleza utamaduni wa kufanya makongamano kila mwaka kwa lengo la kumuenzi muasisi wa Zanzibar na pia kuwakumbusha vijana historia ya Zanzibar ya sasa kupitia mchango mkubwa uliotolewa na Mwasisi wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Mwenyekiti wa Kongamano hilo alikuwa Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho ambapo watoa mada walikuwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Said Ali ambae alitoa mada kuhusu “Fikra za Abeid Amani Karume na mapinduzi ya Uchumi Zanzibar” na Mhe. Mohamed Seif Khatib ambae alitoa mada kuhusu “Fikra za Abeid Amani Karume katika kujenga umoja na mshikamano wa kijamii Zanzibar.
Wadau mbali mbali wakiwemo baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walishiriki na kuchangia katika mada hizo.
Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Shein aliwatunuku vyeti na zawadi wanafunzi wa skuli za msingi na sekondari Zanzibar ambao walifanya vizuri katika shindano la uandishi wa insha kuhusu mchango wa Sheikh Abeid Amani Karume katika maendeleo ya Zanzibar.
Hayati Sheikh Abeid Amani Karume alifariki April 7, 1972.

No comments :
Post a Comment