Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, April 6, 2018

Kitwanga: Ukiwa msema Ukweli lazima wakuondoe!

Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga amefunguka na kusema kuwa mtu ukiwa msema ukweli lazima wakuondoe katika nafasi yako kwa kuwa hawataki watu wasema kweli.Kitwanga amesema hayo bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019, mjini Dodoma na kudai hata ukiwa mtenda haki kwa kila mtu lazima wakuhamishe.

"Kichwa changu na kichwa cha Jenista Mhagama ni vichwa viwili tofauti kabisaa na uwezo wetu wa kufikiri upo tofauti kabisaa, kwa hivyo ni vyema tukapima na kuhakikisha kwamba pale anapofaa Jenista Mhagama aende Jenista Mhagama, pale anapofaa Kitwanga aende Kitwanga lakini hii ya kubebe jumla jumla na wakati mwingine ndugu zetu hii tabia ife na mimi siwezi kukubaliana na hilo na bahati nzuri ukiwa msema ukweli hata ukikaa pazuri watakuondoa tu. Na ukiwa unatenda haki kwa kila mtu hata ukikaa Kolomije watakuondoa wakupeleke Mtwara" alisisitiza Kitwanga.

No comments :

Post a Comment