Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 23, 2018

Mwili wa Leyla Mtumwa wawasili Tanzania kutoka Uingereza!

Mwili wa Mtanzania, Leyla Mtumwa anayedaiwa kuuawa kwa kuchomwa visu na mumewe, Kema Kasambula, mwezi uliopita jijini London nvhini Uingereza umewasili nchini leo Jumatatu, Aprili 23, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kupelekwa nyumbani kwao. Arusha kwa ajili ya shughuli ya mazishi.. 

Mwili wa Leyla ulikuwa ukishikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uingereza kwa ajili ya uchunguzi zaidi na baada ya kujiridhisha ndipo wakaukabidhi kwa familia. Leyla anadaiwa kuuawa na mumewe huyo, usiku wa kuamkia Machi 30, mwaka huu jijini humo ambapo sasa jamaa huyo anakabiliwa na kesi ya mauaji. 

 Leyla ni mtoto wa Hidaya aliyeimbwa na Pepe Kalle kwenye wimbo wake wa Hidaya miaka ya 1990, mwenye makazi yake Kaloleni jijini Arusha ambako ndiko msiba ulipo. Taratibu za mazishi ya Leyla zitaanza kufanyika kesho Jumanne nyumbani kwao Arusha.

No comments :

Post a Comment