Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 23, 2018

TCRA imewapa wamiliki wa blogu wiki mbili kujisajili!

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA ) imewapa muda wa wiki mbili wamiliki wa mitandao ya kijamii ya 'blogs', tovuti na aina nyingine ya vyombo vya habari vya habari vinavyochapisha kwenye mtandao kujisajili nchini Tanzania.Hatua hii imekuja ili kudhibiti maudhui mitandaoni ikiwa ni matakwa ya sheria mpya ambayo ilionekana kuwa na mkanganyo.

Ikiwa sehemu ya usajili, wachapishaji wote wa kwenye mtandao kwa maandishi, video na sauti wanapaswa kulipa dola 1000.

Aidha wachapishaji wa mtandao huo wanatakiwa kuhakikisha wanakamilisha vigezo vyote ambavyo wanatakiwa kuainisha ikiwa ni pamoja kuweka mfumo wakukagua taarifa zisozoruhusiwa katika mitandao na kuweka rekodi ya watumiaji wote, vikiwemo vitambulisho vyao na anuani za wasambazaji wa intaneti.

Atakaye kiuka vigezo muhimu vilivyowekwa atapata adhabu ya kulipa faini isiyopungua dola 2000 au kufungwa jela kwa muda usiopungua mwaka mmoja au adhabu zote kwa pamoja.

Wanaharakati wengi, watumiaji wa mtandao na wamiliki wa mitandao hiyo wameona serikali imeamua kutumia mwanya huo ili kubana uhuru wa kujieleza.

Lakini serikali ya Tanzania inasema imeamua kuchukua maamuzi hayo ili kulinda taifa na maudhui kutoka nje au ndani ya nchi ambayo hayahitajiki katika jamii.

No comments :

Post a Comment