dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, May 13, 2018

Hakutakuwa na Upungufu wa Sukari- Dkt Tizeba!

Waziri wa kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba
Na Bashiri Salum, Dodoma
Serikali imeagiza sukari kiasi cha tani 70,354.35 kutoka nchi za nje lengo likiwa ni kujipanga ili kuhakikisha kuwa hapatokei upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni waziri wa kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa tani 60,539.35 ya sukari itaanza kuingia hapa nchini katikati ya mwezi Mei 2018 ambapo kiasi kilichobaki cha tani 9,815 kitaingia mwezi June mwaka 2018.Aidha Dkt. Tizeba amefafanua kwamba hakutarajiwi kuwa na upungufu wa sukari hapa nchini kwa sababu hadi kufikia tarehe 10 mei 2018 katika maghala ya wazalishaji na wafanyabiashara kulikuwa na tani 78,147.67 za sukari na kiasi kingine tani 25,441.25 kipo Bandarini .

Kwa kiasi cha sukari ambacho tayari kipo hapa nchini kikijumlishwa na kiasi ambacho kitaingia hivi karibuni kutoka nje ya nchi ni dhahiri kwamba nchi haiwezi kupata upungufu wa bidhaa hiyo, alisema Mhe.Waziri.

Awali Dkt.Tizeba alisema kwamba mahitaji ya sukari nchi nzima ni tani 630,000 ambapo kati ya hizo, tani 145,000 ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani na tani 485,000 ni kwajili ya matumizi ya kawaida.

Hata hivyo mapitio yanaonesha kwamba msimu wa mwaka 2017/18 viwanda vya ndani vilizalisha tani 306,226 za sukari kwa matumizi ya kawaida ambapo mwisho wa msimu huu uzalishaji umefikia tani 307,481.76 aliongezea Dkt. Tizeba.

Akimalizia taarifa yake Mhe. Tizeba amebainisha kuwa kwa kiasi ambacho sukari imeagizwa kutoka nje Pamoja na viwanda vya ndani inadhihirisha kwamba hakutakuwa na upungufu wa aina yeyote ya sukari hapa nchini na ikizingatiwa kuwa viwanda vitaanza uzalishaji mwingine mwezi mei ambapo ukarabati (services ) itakuwa imekamilika.

No comments :

Post a Comment