Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla.
Pita kila siku kwa habari moto moto.
(This blog is about Tanzania and the world as a whole.
Pass-by everyday for breaking news).
***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
AirFreight
Kwarara Msikitini
Dual Citizenship #2
Pemba Paradise
Zanzibar Diaspora
ZanzibarNiKwetuStoreBanner
Mwanakwerekwe shops ad
ZNK Patreon
Scrolling news
Tuesday, May 29, 2018
Prof. Lipumba azuiwa na Mahakama!
Mahakama Kuu ya Tanzania imemzuia Jaji Francis Mutungi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini au Wakala wake yeyote yule kutoa fedha za ruzuku za Chama cha Wananchi (CUF), na kumpa Prof. Ibrahim Lipumba mpaka hapo mashauri ya msingi yanayoendelea Mahakamani yatakaposikilizwa.
Zuio hilo limetangazwa leo Mei 29, 2018 na Jaji Wilfred Dyansobera katika Mahakama hiyo na kusisitiza kwamba, maombi ya CUF ya kulinda fedha hizo yana nguvu za kisheria. Taarifa za chama zinaeleza kuwa hadi amri hiyo ya Mahakama inatolewa, Jaji Mutungi na Ofisi yake ya Msajili wa Vyama imeshamruhusu Prof. Lipumba kuchukua zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 na fedha hizo zimekuwa zikiwekwa kwenye akaunti zisizotambuliwa na Bodi Halali ya Udhamini ya chama na kisha kuhamishiwa kwenye akaunti za watu binafsi akiwemo Prof. Lipumba Mwenyewe.
Shauri kuhusu uhalali wa Bodi ya Wadhamini linaendelea kusikilizwa na inatarajiwa kuwa shahidi wa tatu wa upande wa Chama ataanza kutoa ushahidi wake mwezi Juni mwaka huu.
No comments :
Post a Comment