dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, June 2, 2018

BINTI MWENYE UWEZO WA KUNUSA HARUFU YA KIFO CHA MTU AZUA GUMZO!

Mwanadada kutoka nchini Australia Ari Kala mwenye umri wa miaka 24 ameibua gumzo baada ya kugundua kuwa ana uwezo wa kunusa harufu ya kifo kwa mtu.
Mwanadada huyo ambaye kwa sasa anasomea taaluma ya saikolojia anasema kuwa aligundua kipaji chake hicho alipokuwa na miaka 12 alipokuwa ameenda kumtembelea mjomba wake aliyekuwa amekaribia kufa na ndipo aliponusa harufu ya kifo ambayo haikutambuliwa na mtu yeyote.
“Nilidhani ni harufu ya mabaki ya mwili wa mjomba kwa sababu ilikuwa harufu mbaya sana ambayo sijawahi kuinusa. Lakini hakuna mtu mwingine aliyeweza kuinusa harufu hiyo” amesema Ari.

Ari ameongeza kuwa baadae alikuja kugundua kuwa mara kwa mara ameweza kunusa kifo na kuna wakati mwingine anaona ni mzigo kuwa na talanta hiyo na huwa anatamani kuwaambia watu wanaotaka kufa kwamba wanakaribia kufa.

No comments :

Post a Comment