Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, July 1, 2018

ZACADIA YAISHUKURU PBZ LTD KWA KURAHISISHA UPELEKAJI WA REMITTANCES TANZANIA!

Jumuiya ya ZACADIA yenye makao makuu yake mjini Toronto, Canada, leo imeishukuru benki ya Watu wa Zanzibar kwa kusaidia huko nyuma kutatua suala lililokuwa gumu kwa muda mrefu la upelekaji wa pesa (remittances) kutoka kwa Wana-Diaspora kuenda nyumbani Tanzania.

Kutokana na msaada huo, leo Tanzania inapokea pesa za kigeni zenye thamani ya mabilioni ya shilingi kila mwezi kupitia huduma iliyoanzishwa na benki hii.

Wakati benki ya Watu wa Zanzibar inasherehekea miaka 52 (1966-2018) tangu kuzaliwa kwake, Jumuiya hio iliandika leo kwenye ukurasa wake wa blog (zacadia.org) na kwenye website yake (zacadia.com) kuwa....

"Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Ltd) inapoazimisha miaka 52, Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi Canada, ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association), inaishukuru benki yetu hii kwa kutuondoshea Wana-Diaspora wote wa Tanzania shida iliokuwa sugu huko nyuma kwa miaka mingi ya kupeleka pesa nyumbani Tanzania (remittances) kutoka ughaibuni. 

Huko nyuma  upelekaji wa pesa nyumbani Tanzania ulikuwa mgumu sana na wengi tukishindwa kutokana na fees za juu ambazo makampuni ya multi-national conglomerates za remittances zilikuwa zikitutoza, mpaka pale Benki ya Watu wa Zanzibar ilipoingilia kati kutatua suala hili na kutuletea njia yenye bei nafuu  kwa kushirikiana na WorldRemit.

Leo tunashukuru kwani sio bei ni nafuu tu, lakini tunaweza pia kupeleka pesa nyumbani Tanzania from the palms of our hands, bila ya kuenda benki kupanga foleni na kwahivyo tunasema... THANK YOU PBZ LTD! 

Zaidi, kwa msaada huu Watanzania wote tunaoishi nje wenye kupeleka pesa nyumbani tunaipa hongera benki ya Watu wa Zanzibar kwa kusherehekea miaka 52 ya kuwahudumia wananchi na tunaitakia maendeleo makubwa zaidi mwaka hadi mwaka". 

"The People's Bank, The People's Choice in the Diaspora!"

Source: Zacadia.org

1 comment :

  1. Hivyo njia hii ya WorldRemit imeletwa na Benki ya Watu wa Zanzibar na sio na Tigo. Ahsante kwa kutujulisha.
    Ni msaada mkubwa kwetu huku majuu. Western Union ikitunyonya na ilikuwa ukienda kwa agents wake utapoteza sio chini ya dakika 30, kwani wapo busy sana na business nyengine.
    Sasa tunawapelekea chochote ndugu zetu Bongo bila ya kuenda benki. Ahsanteni Benki ya Watu Wa Zanzibar!
    Ingelikuwa vizuri pia kama Watanzania nao wa huko nyumbani wangeweza kuwapelekea school fees watoto wao nje bila ya kuenda benki - litizameni na hili wana-benki ya Unguja.

    ReplyDelete