dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 24, 2018

DR Congo yazikataa AU, UN kusimamia uchaguzi wao!

Vizingiti vya kila aina vinaizonga Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo miezi minne tu kabla ya uchaguzi utakaoamua hatima ya nchi hiyo ambayo ni mojawapo ya nchi zinazozongwa na mizozo ya kila aina ulimwenguni..

Umoja wa Mataifa, Afrika Kusini, Umoja wa ulaya na wengineo, wote hao DRC inasema haihitaji msaada wao, ushauri wao wala maoni yao kuhusu maandalizi ya uchaguzi uliopangawa kuitishwa Desemba 23 inayokuja.Kinshasa inataka kuwaweka kando "wajumbe maalum" na wasimamizi wengineo, na zoezi la uchaguzi ambalo lengo lake kuu ni kupatikana kwa mara ya kwanza kipindi  cha mpito kwa njia ya amani nchcini humo.

Hadi wakati huu ratiba inaheshimiwa tangu rais Joseph Kabila aliposema hatogombea tena na badala yake kumteuwa "mfuasi wake". Orodha ya muda ya wagombea inatarajiwa kutangazwa wakati wowote hii leo.

Jumatatu iliyopita viongozi wa mjini Kinshasa walipinga ripoti iliyotangazwa na vyombo vya habari, bila ya kuthibitishwa na serikali kuhusu kuteuliwa rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki kuwa "mjumbe maalum" katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

"Nnaweza kukwambieni, hakutokuwepo tena na mjumbe maalum yeyote katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, hata kama ni Thabo Mbeki" alisema mshauri wa masuala ya kidiplomasia wa rais Kabila, Barnabé Kikaya Bin Karubi.

Anawalaumu  wajumbe hao  na kudai wana mtindo wa kujigeuza "mabalozi wadogo", hawaheshimu mamlaka ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo."Tunataka kudhihirisha tuko huru", amesema kwa upande wake waziri wa mawasiliano Lambert Mende.

No comments :

Post a Comment