dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 23, 2018

HATIMAYE MKURUGENZI WA UCHAGUZI KOROGWE AKUBALI KUPOKEA RUFAA YA CHADEMA!

Rufaa ya mgombea ubunge wa Jimbo la Korogwe (Chadema) Amina Saguti imepokewa jana  na Kaimu Mkurugenzi wa uchaguzi Wilaya ya Korogwe, Florian Kimaro.

Hii ni Taarifa iliyotolewa jana Agosti 22 na Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene 

Hatimae fomu ya rufaa ya Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia CHADEMA, Bi. Amina Ally Saguti imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Korogwe, Ndugu Frolian Kimaro baada ya malumbano marefu, ambapo mamlaka zinazohusika zilikuwa zimekataa kuipokea.

Katika rufaa hiyo Mgombea Bi. Saguti anapinga, pamoja na masuala mengine, uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe Vijijini kumtangaza mgombea ubunge wa CCM kuwa amepita bila kupingwa, huku kukiwepo na ukiukwaji mkubwa wa taratibu zinazosimamia uchaguzi nchini.

Hadi mwisho wa kupokea rufaa hiyo ulipokuwa unakaribia jioni hii, kwa mara nyingine tena uteuzi wa mgombea huyo wa CHADEMA ulikuwa bado unawekewa vikwazo baada ya Msimamizi wa Uchaguzi kukataa kupokea fomu hiyo tangu mchana.

Mgombea huyo akiambatana na Viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Korogwe, walifika ofisini kwa msimamizi leo mchana kuwasilisha fomu hizo lakini alikumbana na vikwazo hali iliyoonesha kuwa kuna dalili za kuhakikisha uamuzi wa juzi haubadiliki ili CCM ipite bila kupingwa katika jimbo hilo.

Fomu hiyo na. 12 ilipatikana  kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya Uongozi wa CHADEMA ngazi ya taifa kulazimika kufanya mawasiliano ili kupata fomu hiyo kutokana na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe kukataa kutoa.

Chama tayari kimeshamwandikia rasmi Mkurugenzi wa NEC kumtaka achukue hatua za haraka kuingilia kati mwenendo wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe hasa kubatilisha uamuzi wake uliokiuka taratibu zinazosimamia uchaguzi kwa kukataa kupokea fomu za kugombea za Mgombea wa CHADEMA na vyama vingine huku akimtangaza Mgombea wa CCM kupita bila kupingwa kinyume cha sheria na kanuni za uchaguzi.

Tumaini Makene

No comments :

Post a Comment