dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 23, 2018

Trump awaonywa wamarekani, " Mkiniondoa uchumi utaharibika"!

Rais wa Marekani Donald Trump amejibu uvumi kuwa anaweza kuondolewa kwa kura ya kutokuwa na imani naye kwa kuonya kuwa uchumi utaharibika

Wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha Fox & Friends alisema masoko yataporomoka na "kila mtu atakuwa maskini".

Alikuwa akizungumza baada ya Michael Cohen, wakili wake wa zamani kukiri kuvunja sheria za uchaguzi na kusema alishauriwa kufanya hivyo na Trump.Si kawaida kwa Trump kuzungumzia suala la kutolewa mamlakani.

Waandishi wa habari wanasema haiwezekani kuwa wapinzani wa Trump watajaribu kumuondoa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye kabla ya uchaguzi wa kati ya muhula wa mwezi Novemba.

Sijui ni kwa njia gani mtamtoa madarakani mtu ambaye amefanya kazi nzuri," Trump alikiambia kipindi cha Fox and Friends.

"Ninawaambia hivi, ikiwa nitaondolewa nafikiri masoko yataporomoka, nafikiri kila mtu atakuwa maskini."

Trump alitetea malipo kwa wanawake wawili na kusema hakuwa anawajua wakati huo.

Matamshi yake yanaenda kinyume na taarifa zilizotolewa mapema na Cohen ambapo alisema kuwa Rais Trump aliimuagiza kufanya malipo hayo.

Mwezi Julai Cohen alitoa kanda ya sauti yake na Trump wakizungumzia moja ya malipo hayo kabla ya uchaguzi

Cohen anasem alifanya malipo hayo kwa wanawake wawili wakati wa kampeni ya urais ya mwaka 2016.

Wanawawe hao wawili wanatajwa kuwa manyota wa filamu za ngono Stormy Daniels na Karen McDougal, wote walidai walikuwa na uhusiano na Trump

Lakini Trump alisisitiza kuwa malipo hayo hayakukiuka sheria za uchaguzi.

Alisema malipo hayo yalitoka kwake mwenyewe na sio kutoka kwa kampeni lakini hakufahamua kuyahusu hadi baadaye.

No comments :

Post a Comment