dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 24, 2018

Lema: “Haki, usawa na utawala havituhusu sisi tu”!

Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA), Godbless Lema.
Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA), Godbless Lema amefunguka kuwa suala la haki, usawa na utawala wa sheria haliwahusu Chadema peke yao bali ni wajibu wa kila mwananchi.

Lema amesema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ambapo amedai kuwa tatizo kubwa linalolikabili taifa kwa sasa ni kuwa wananchi wanadhani kuwa haki na demokrasia inatafutwa na wapinzani pekee.“Watu wanafikiri masuala ya haki, usawa na utawala wa sheria ni wajibu wa CHADEMA hawa wana hitaji maombi na dua,jambo lolote linalohusu haki na demokrasia ni wajibu wa kila Mwananchi.Tatizo kubwa linalokabili Nchi kwa sasa ni kuwa na aina hii ya fikra hata kwa wanaoitwa wasomi”, ameandika Lema.

Kauli ya Lema imekuja ikiwa ni siku moja toka Menyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo taifa (CHADEMA), Freeman Mbowe kufunguka kuwa kudai kuwa hawaridhishwi na mwenendo wa kesi inayowakabili.

No comments :

Post a Comment