Katika kuhakikisha kitendo kilichotokea mkoani Kagera cha mwanafunzi kupigwa na kusababishiwa kifo hakitokei mkoani Tanga, mkuu wa mkoa huo Martine Shigela amewaagiza viongozi wa mkoa huo kusimamia sheria za adhabu mashuleni.
Akiongea leo kwenye kikao cha robo ya tatu ya mwaka cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC), Shigela amesema mwalimu atakayebainika kutoa adhabu kinyume na utaratibu naye aweze kuadhibiwa kama ilivyokuwa kwa mwanafunzi.
''Mwalimu akienda kinyume na sheria ya adhabu mashuleni maana yake kajitengenezea sheria yake ambayo haijatungwa na bunge hivyo kwa kosa hilo lazima iwepo adhabu kwa mwalimu aliyevunja sheria na kwasababu anakuwa ametoa adhabu ya viboko ni vyema na yeye akapata viboko kama alivyo mchapa mwanafunzi'', amesema.
Kwa upande wake afisa elimu mkoa wa Tanga Mayasa Hashim amewaasa walimu kufuata utaratibu wa aina ya adhabu anazopaswa kupewa mwanafunzi huku akiongeza kuwa sio kila kosa linahitaji adhabu bali makosa mengine yanatakiwa kuishiwa kwa mwalimu kumshauri mtoto ili asirudie.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment