zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 21, 2018

LHRC yaijibu Takukuru, yaitaka kufuata sheria na siyo kutoa matamko!

Kufuatia Taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali NGO'S kutakiwa kupeleka taarifa zao za misaada kutoka kwa wafadhili wake na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru), leo Kituo cha Haki na Binadamu LHRC wamejitokeza kujibu wakiitaka Serikali kuunda kwanza sheria.
Anna Henga ambaye ni Mkurugenzi wa LHRC amesema wamelisikia agizo hilo lililotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Julius lakini akaitaka serikali itunge sheria hiyo kwanzaa na sio kutoa tamko ambalo halina uhalali wa kikatiba.

Amesema wao kama LHRC wanajiamini na wamekuwa wakitoa taarifa zao za mapato kila mwaka lakini hawawezi kutoa taarifa za fedha wanazopatiwa na wafadhili wao kwani hakuna sheria ambayo inawabana kuwasilisha taarifa hizo takukuru.

" Hatukatai kupeleka taarifa zetu za wafadhili eti kwa sababu tunahofia chochote, bali tunachohitaji sisi ni kuona tunazipeleka kihalali kwa kufuata sheria, sasa kama sheria haipo basi LHRC hatuwezi kutoa taarifa zetu za fedha tunazopewa na wafadhili hadi pale sheria itakapotungwa," amesema Anna.

No comments :

Post a Comment