
Marais watatu wa zamani nchini Madagascar kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba 7, wakati huo huo rais aliemadarakani ametangaza kujiuzulu ili aweze pia kushiriki katika uchaguzi.
Kutokana na katiba ya nchini humo haimpi ruhusu rais aliemadarakani kuwania kiti cha urais hadi ajiuzulu siku 60 kabla ya tarehe iliopangwa kufanyika uchaguzi .
Marais wa zamani wanaogombea kiti cha urais katika uchaguzi ni Andry #Rajoelina ambae aliongoza mwaka 2009 hadi mwaka 2013, Marc Ravolamanana (2002 -2009) na Didier Ratsiraka ambae ana umri wa miaka 81, Ratsiraka aliongoza Madagascar (1975- 1993) na (1997 -2002).
No comments :
Post a Comment