Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 21, 2018

Ndugu yake Bobi Wine akamatwa Kampala Uganda!

Nduguye mbunge wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine Eddy Yawe na Naibu msemaji wa chama cha Democratic party Waiswa Alex Mufumbiro, wamekamatwa na Vikosi vya usalama na kuzuiwa kwenye kituo cha Polisi Uwanja wa Entebbe.

Ripoti pia zinasema kuwa kila mtu wa familia anayewasili uwanja wa Entebbe anakamatwa, licha ya polisi kusema awali kuwa watawaruhusu watu wa familia kumkaribisha Bobi Wine.

Kwa sasa vikosi vya polisi mjini Kampala viko kwenye tahadhari kubwa kabla ya kuwasili kwa mbunge huyo wa Kyadondo East.

Bobi Wine anatarajiwa kuwasili Kampala alasiri, leo Alhamisi kutoka nchini Marekani ambapo alikuwa ameenda kupata matibabu baada ya kuripotiwa kuteswa na vikosi vya usalama.

Akiwa nchini Marekani Bobi Wine alifanya mikutano kadhaa na waandishi wa habari na kuhojiwa na vituo vingi vya televisheni za kimtaifa.

Tangu atangaze kurudi Uganda, makamanda wa polisi mjini Kampala wamekuwa wakifanya mikutano tangu Jumatatu kujiandaa kurudi kwa mbunge huyo.

Zaidi ya watu 1000 wanatarajiwa kufurika barabara ya Entebbe kumkaribisha Bobi ambaye ana wafuasi wengi vijana.

Taarifa za polisi zilisema kuwa vikosi vya kupambana na ghasia vimepelekwa kwenye barabara ya Entebe, katikati mwa mji wa Kampala, Kamwokya (alikokulia Bobi Wine na Kasangati.

Bobi Wine aeleza madhila yake
Kiwango kikubwa cha polisi kimepelekwa kwenye barabara ya kutoka Kampala kwenda Entebbe ambapo watu wanaweza kukusanyika kumuona Bobi Wine.

Polisi wanasema Bobi Wine hajapewa kibali cha kufanya mkutano au shughuli yoyote.

Msemaji wa polisi mjini Kamapala Luke Owoyesigyire, alionya kuwa yeyote ambaye atashiriki kwenye shughuli yoyote inayomhusu Bobi Wine atakamatwa

Kwenye video aliyochapisha kwenye mtandao wa Facebook, Bobi Wine anasema serikali inapanga kuzua ghasia ili kuwalaumu wafuasi wa chama cha People Power.

Kulinganga na Bobi, baadhi ya watu wanachapisha shati nyekundu za wafuasi wa People Power na kuwapa majangili wa serikali ili wapate kuzua ghasia ndio waonekane kuwa wao ni wafuasi wake.

No comments :

Post a Comment