Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha wakala wa Serikali wa uchapaji Zanzibar Nd,Mohamed Suleiman alipofanya ziara leo ya kutembelea katika Ofisi hiyo iliyopo Maruhubi Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi.
Na.Rajab Mkasaba Ikulu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein alitembelea Ofisi ya Wakala wa Serikali wa Uchapaji Zanzibar iliyopo Maruhubi nje kidogo ya mji wa Zanzibar na kusisitiza haja ya kuchapishwa kopi nyingi za Gazeti la ‘Zanzibar Leo’ ambalo ni gazeti la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alieleza kuwa ipo haja ya kuliimarisha zaidi soko la ndani la gazeti hilo kabla ya kuliimarisha soko la nje huku akitumia fursa hiyo kueleza uwezo mkubwa wa kiwanda hicho ambacho kina mashine mpya na za kisasa ambazo hakuna kiwanda hata kimoja cha binafsi hapa nchini chenye mashine hizo.Aidha, Rais Dk. Shein alieleza kuwa katika kwianda hicho kuna mashine ambazo katika bara la Afrika ni viwanda vichache ambavyo unaweza kuzikuta mashine hizo ambapo kwa hivi sasa mashine hizo kwa upande wa gazeti zina uwezo wa kuchapishwa magazeti kopi 30,000 kwa saa moja.
Alisisitiza kazi kubwa ya kuliuza gazeti hilo na kuhakikisha wananchi waliowengi wa Unguja na Pemba wanapata gazeti hilo na kuhakikisha asilimia kumi ya wananchi wa Zanzibar wanapata gazeti hilo. Mapema Dk. Shein alipata fursa ya kukagua eneo hilo la Ofisi ya Wakala na kuziona mashine zake.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments :
Post a Comment