Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani nchini Tanzania Edward Lowassa amesema kuwa nguvu za chama cha upinzani cha Chadema zinaendelea kuimarika na kwamba upinzani utashinda uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Monduli.
Akizindua kampeni za Chadema katika eneo bunge hilo katika wadi ya Mto wa Mbu , Lowassa aliwataka wakaazi kufutilia mbali uvumi kwamba chama hicho cha upinzani kilikuwa kinaendelea kufa.Alisema kuwa katika huduma yake ya miaka 20 kama mbunge wa Monduli alikabiliana na matatizo mengi yanayowakabili wakaazi wa eneo bunge hilo.
Alisema kuwa miundo mbinu iliimarika, kulikuwa na umeme na alitatua matatizo mengi yaliokuwa yakiwakumba wakaazi wa eneo hilo.
Alisema kuwa upinzani unazidi kuimarika na kwamba utaibuka mshindi wakati wa uchaguzi mdogo.
Kuhusu wanasiasa wa upinzani kuhamia serikalini, anasema kuwa alikasirishwa na hatua hiyo hususan ile ya mbunge wa Monduli Julis Kalanga kuhamia CCM.
Lakini licha ya Lowassa kutoa kauli yake kwamba upinzani unaimarika, hatua za hivi majuzi za wabunge wa upinzani kujiunga na CCM ni swala linalowashangaza raia wengi wa Tanzania. Iweje kwamba upinzani unazidi kuimarika huku viongozi wake wakionekana kujiunga na chama tawala?
Miaka ya nyuma mwanasiasa akihama katika chama chake ilikuwa ni jambo zito sana, lakini kwasasa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vimegubikwa na taarifa za wanasiasa wanaohama vyama vyao mara kwa mara.
Kwa zaidi ya wiki moja mfululizo wanasiasa ikiwemo wabunge na madiwani kutoka chama cha CUF na Chadema walitangaza kujiengua katika vyama vyao ikiwemo kujiuzulu nafasi zao za uongozi.
Naibu meya wa manispaa ya ilala, na diwani wa vingunguti Omari kumbilamoto amejiuzulu nafasi ya udiwani na umeya lakini pia amejivua uanachama wa CUF.
Mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Julius Kalanga Laizer amejiuzulu na kujiunga na CCM kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.
Kabla ya kalanga kujiuzulu alikuwa ni mwanasiasa wa upinzani, Mwita Waitara alitangaza kujiengua katika chama kikuu cha upinzani cha chadema na kujiunga na Chama tawala, CCM.
Waitara aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ukonga lililopo Dar es salaam alikishutumu chama cha Chadema, kuwa hakina demokrasia pia kutokuwa na maelewano na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.
Ikumbukwe kuwa wabunge hawa wote yaani Waitara na Kalanga waliwahi kuitumikia CCM, ambapo Waitara aliitumikia CCM mwaka 1998 mpaka mwaka 2008 wakati Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM.
Sheria inasemaje
Kwa mujibu wa sheria wanasiasa hawa, wabunge, madiwani na Meya wamejiengua katika nyadhifa zao zote walizopata katika uchaguzi mwaka 2015, hivyo majimbo yao yako wazi.
Hata hivyo baada ya kujiengua baadhi yao wamepata neema ya kuteuliwa na rais katika baadhi ya nafasi za uongozi. Wiki iliyopita Rais Magufuli alimteua David Kafulila kuwa katibu tawala wa mkoa wa Songwe.
Pia alimteua Moses Machali kuwa mkuu wa wilaya ya Nanyumbu. Kabla ya uteuzi huo Machali aliwahi kuwa mbunge wa Kasulu mjini kupitia NCCR-Mageuuzi ambapo baadaye alihamia ACT-Wazalendo kisha kwenda CCM.
Mwanasiasa mwingine aliyepata fursa hiyo ya kuteuliwa na Rais ni Patrobas Katambi ambaye amekuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma, Kabla ya hapo Katambi alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la vijana la Chadema.
Lakini pia kitendo cha Muheshimiwa Rais wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli kuwateua baadhi ya viongozi waliotoka upinzani kina maanisha nini?
BBC imefanya mazungumzo na Dotto Kuhenga, mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Tanzania.
"Mpaka sasa miaka zaidi ya 20 bado hakuna uelewa wa kutosha sana kuhusu nini maana ya siasa za ushindani wa vyama vingi. Hii ni kwa viongozi na hata kwa wananchi wa kawaida" Kuhenga anaiambia BBC.
Lakini pia mchambuzi huyo amezungumzia swala la vyama vya siasa kutoweka nguvu katika uwekezaji wa kutosha kwenye uelewa wa itikadi za vyama husika.
"Viongozi wengi sana iwe ni katika chama tawala cha CCM, iwe katika vyama vya upinzani ukitazama wale ambao wameivishwa wakameza zile itikadi na wakaziishi zile itikadi za vyama vyao ni wachache sana, utakuta wengi wataongelea namna walivyokuwa katika vyama Fulani, Fulani alikuwa anafanya hivi na hivi. Huwawe ukawasikia wanaelezea kwa undani maswala ya itikadi za vyama vyao ilani za vyama vyao zinasema nini na kwanini wametofautiana na ilani hizo," anasema Dotto Kuhenga.
Maslahi ya kibinafsi
Hata hivyo mchambuzi huyo anaongeza kuwa kumekuwa na uelewa mkanganyiko juu ya nini maana ya uongozi, huku akigusia swala la kuweka mbele maslahi binafsi.
"Uongozi hivi sasa, uwe ni ubunge watu wengi wanaangalia kwanza maslahi yao sio maslahi ya wananchi. Ukiangalia miaka ile ya zamani kulikua na kuangalia zaidi maslahi ya wananchi, lakini sasa kuna huu mgongano mkubwa wa maslahi ya mtu binafsi kama kiongozi na maslahi ya wananchi"
Magufuli: CCM itatawala milele Tanzania
Kuhenga amemaliza kwa kusema,hayo mambo matatu yamekuwa ni chagizo la haya yanayo tokea kwa sasa.
Ikumbukwe kuwa, tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 nchini Tanzania, kumekuwa na wimbi la wanasiasa hasa wabunge na madiwani wa upinzani kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na chama tawala huku baadhi ya wabunge wa chama tawala wakihamia upinzani.
Kujiuzulu kwa wanasiasa hao kunasababisha serikali kutumia mamilioni ya fedha za walipa kodi kugharamia uchaguzi wa marudio katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments :
Post a Comment