zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 18, 2018

Utata umekwisha! Mafahari wawili Korea Kusini na Kaskazini wakutana!

HAKUNA ugomvi! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Viongozi wa Korea Kusini na Kaskazini kukutana mjini Pyongyang, Korea Kaskazini kujadiliana kuhusu kuondoa silaha za nyuklia kwenye rasi ya Korea na masuala mengine ambayo yamekuwa kiini cha mzozo baina yao.

Rais Moon Jae-in wa Korea kusini aliwasili Pyongyang kwa mkutano huo wa tatu kwa mwaka huu na kupokelewa na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un.

Kabla ya kuanza kwa mkutano wao wa kilele Rais Moon Jae in na mwenzake wa kaskazini Kim Juong un walitumia gari la pamoja kukatisha katikati ya mji mkuu wa korea kaskazini Pyongyang ambapo maelfu ya raia waliojipanga barabarani waliwashangalia wakisema ‘Muungano wa taifa' na kupeperusha bendera za nchi zote mbili kuashiria haja ya kuungana tena.

Nchini korea kusini lakini mkutano huo umeandamwa na maadamano ya wananchi wanaopinga ushirikiano wa karibu na Korea kaskazini.

Moon ambaye aliwasili Pyongyang siku ya jumanne alilakiwa kwa gwaride la kijeshi na heshima ya zulia jekundu mbele ya mwenyeji wake Kim Jong Un ambaye uwepo wake katika uwanja wa ndege umetajwa na vyombo vya habari kuwa jambo la kushangaza.

No comments :

Post a Comment