Hayo ameyaeleza wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja MHE, Ayoub Mohammed Mahmoud katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Amani duniani ambapo madhimisho hayo Zanzibar yalifanyika katika viwanja ya kumbukumbu ya Mapinduzi, kisonge mjini Magharib Unguja.
Mhe, Meya alisema vijana ndo kundi linalohitajika kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kudumisha amani ya nchi kwani wanasiasa pamoja na kundi la watu wasiopendelea mema nchi hupendelea kuwatumia vijana katika kubomoa na kuichafua amani ya nchi na mwishoe kuingia katika migogoro ya wenyewe kwa wenyewe.
“Zanzibar tumekuwa ni miongoni mwa nchi zilizopata fursa ya kuadhimisha siku hii muhimu ambapo ni kielelezo kuwa nchi yetu ina Amani hivyo tunatakiwa kutunza na kuenzi amani iliyopo nchini” Alisema Naibu Meya.

Alisema ili kuendelea kudumisha Amani iliyopo nchini jamii inatakiwa kuwa wavumilivu wenye kuridhiana pamoja kustahamiliana kwa mambo yote ambayo wamekoseana au kukwazana kwa namna moja au nyingine.
Aidha Mhe,Meya alihimiza Jamii kuanzisha vilabu mbali mbali vyenye lengo la kulinda na kutunza amani ya nchi huku vilabu hivyo vikiwa nahamasisha na kuelimisha makundi tofauti katika Nyanja ya kisiasa, uchumi,michezo na kijamii.
Mapema akisoma risala kwa mgeni rasmi Tatu Abdallah Msellem kutoka Katika Taasisi ya Amani UKweli na Uwazi Zanzibar alisema kupitia jumuiaya yao wanatumia siku hii katika kuamsha ufahamu, Ari na haja ya kuwa na amani kwa Zanzibar, Tanzania na duniani kote.
“tuna amini kuwa siku hii ikitumia ipasavyo jamii ikapata ujumbe wa kulinda na kutunza amani tunaweza kufikia malengo ya umoja wa mataifa ya kutaka amani itawale duniani kote” alisema msoma risala Tatu Abdallah mselem.
Nae mratibu kutoka Taasisi ya Mimi na Wewe Foundation Ali Abdallah Natepe alisema jamii inatakiwa kutunza amani iliyopo nchini ili zanzibar na Tanzania kwa ujumla iendelee kutajwa kwa sifa hiyo nzuri ya kuwa ni kisiwa na kitovu cha Amani Duniani.
“Nchi yetu imekuwa ikitajwa kuwa ni sehemu yenye Amani na utulivu hivyo kama wazanzibar, watanzania tusikubali sifa hizi ziweze kutoweka” alisema Ali Natepe
Hata hivyo alisema kupitia Taasisi yao ya MIMI NA WEWE foundation kila shughuli wanazofanya huwa za kusaidia jamii katika Afya, Elimu, Michezo huwa wanasisitiza jambo la msingi la kutunza na kulinda amani.
Kila ifikapo tarehe 21 mwezi wa tisa kila mwaka huadhimishwa siku ya amani duniani ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu yake “kamwe hatutaweza kuwa na amani ya kweli mpaka tutakapo kuwa tumeondoa chuki katika mioyo yetu”
Kilele cha maadhimisho ya siku hii ya amani duniani imefanyika katika viwanja vya Mapinduzi square mjini magharib Unguja na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali.
Wakati huo huo Zanzibar ikiwa inadhimisha siku ya amani duniani huku Tanzania kwa ujumla ikiwa na simanzi na majonzi ya kuwapotea ndugu zao kwa tukio la kuzama kwa meli ya MV NYERERE iliyotekea katika ziwa Victoria, MUNGU AZILAZE Roho za marehemu mahari pema peponi.

No comments :
Post a Comment