Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 21, 2018

Wanaopinga uhalali wa muungano wa Tanzania wapata pigo!

Mahakama ya Afrika Mashariki imetupilia mbali ombi la raia wa Zanzibar waliowasilisha kesi kupinga uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka kesi hiyo isikiliziwe Zanzibar.

Rashid Salum Adiy na wenzake 39,999 kutoka Zanzibar wamewasilisha kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania wakisema muungano huo ni haramu.

Walalamishi walikuwa wamejitetea kwamba wengi wao ni wakazi wa Zanzibar na huenda ikawa vigumu kwao kuhudhuria vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo iwapo itaendelea kusikiliziwa Arusha.

Ombi hilo limetupiliwa mbali na majaji katika mahakama hiyo mjini Arusha, ingawa hawakutoa maelezo kuhusu sababu zilizowaongoza kutoa uamuzi huo.

Katika uamuzi wake, majaji walisema hakuna haja na wala haifai kwa mahakama hiyo kuagiza kwamba vikao vya kesi hiyo viandaliwe Zanzibar.

Kifungu 68 cha sheria za mahakama hiyo kinawaruhusu kutoa uamuzi kwanza na kisha kutoa maelezo ya kina baadaye.

Wameahidi kutoa maelezo ya kina baadaye.

Katika kesi hiyo, Salum na wenzake wawawameshtaki miongoni mwa wengine Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Serikali ilitetewa na jopo la mawakili wakiongozwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt Ally Possi.

Mwezi Machi, mahakama hiyo ilikuwa imetupilia mbali ombi la walalamishi la kutaka kumteua Japheth Kiziba kuwa mwakilishi mpya mahakamani.

Majaji wakiongozwa na Jaji Monica Mugenyi walilalamikia walichosema ni ishara za walalamishi kutochukulia kwa uzito kesi waliyokuwa wameiwasilisha, wakizungumzia moja ya maombi yaliyokuwa yamewasilishwa.

"Hii ni kama kuipotezea muda mahakama hii na ni hatua ambayo imesababisha kuchelewa kusikizwa kwa kesi hii, na pia ni kutumia vibaya mchakato wa mahakama," walisema majaji.

Wakati mmoja, walalamishi walijaribu kutumia lugha ya Kiswahili, jambo ambalo mahakama hiyo mwezi Machi ilisema linaenda kinyume na mkataba wa kuundwa kwa mahakama hiyo Kifungu 46 ambacho kinasema lugha ya Kiingereza ndiyo lugha pekee ya jumuiya hiyo.

No comments :

Post a Comment