Mhe. Balozi Meja Jenerali Issa Nassor alizungumza na kujadiliana na Wafanyabiashara hao umuhimu wa kuimarisha biashara na kuwekeza nchini Tanzania katika sekta za viwanda, kilimo, uvuvi, madini, utalii, miundombinu, ujenzi wa nyumba za bei nafuu (real estate) na maeneo mengine ya uwekezaji.
Mkutano huo uliandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Misri kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania na Jumuiya ya Wafanyabiashara ya Misri.
Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Misri walihudhuria akiwemo Balozi Wael Abel, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri.
Aidha, majadiliano kwa upande wa wafanyabiashara yaliongozwa na Dkt. Sharrif EL Ghaby, Mwenyekiti wa Kamati ya Afrika katika Jumuiya hiyo akishirikiana na Bw. Mohamed Yusri, Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Misri (Egyptian Businessmen Association).
Hatua hizi ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania inayosisitiza diplomasia ya uchumi, ilani ya uchaguzi ya chama tawala na mkakati wa Serikali katika kufanya mapinduzi ya uchumi katika kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 unaoshajiishwa na viwanda.

No comments :
Post a Comment