Kufuatia kikao cha kamati kuu CHADEMA kilichokaa jana kufuatia kusambaa kwa ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wenye kuasharia utovu wa nidhamu inayowahusisha Wabunge wawili Saed Kubenea na Anthony Komu (CHADEMA) kimewakuta na hatia baada ya kukiri mbele ya kamati hiyo.
Akizungumza mbele ya wanahabari Naibu Katibu Mkuu Bara John Mnyika amesema kuwa wabunge hao wamekutwa na hatia na wamepewa onyo kali ambapo wametakiwa kuandika barua ya kuomba radhi kwa chama, wamewekwa kwenye uangalia ndani ya miezi 12, wamevuliwa nafasi zote za uongozi ndani ya chama na kubaki na nafasi moja ya uwakilishi kwa wananchi, pia wametakiwa kujitokeza mbele ya umma kupitia vyombo vya habari kuomba radhi kutokana na sakata hilo.
Kwa upande wake Saed Kubenea amekiri na kuomba radhi mbele ya waandishi wa habari na kuahidi kuendele kukijenga chama hicho.
Nae Anthony Komu amesema swala hilo ni la kiubinadamu kama unavyoona gari linavyofeli breki hivyo wataendelea kukitumikia chama hicho kama kawaida.

No comments :
Post a Comment