Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimekanusha taarifa zinazosambaa za kutofautiana kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji katika vikao vya kamati kuu.
Taarifa inayosambaa inasema wawili hao walitofautiana katika kikao hicho kilichofanyika nyumbani kwa Mbowe ambacho kilikua na lengo la kujadili mwenendo wa wabunge wake wawili, Saed Kubenea wa Jimbo la Ubungo na Anthony Komu wa Moshi Vijijini.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Mkurugenzi wa Itifaki Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema amesema taarifa hizo ni za uongo na zina lengo la kupotosha na kuongeza kuwa hakuna kikao chochote cha kamati kuu ambacho kimefanyika mwishoni mwa juma lililopita.
" Ni mambo ya kutunga tu au niite ni uzushi, hakuna sehemu yoyote ambayo Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu wamepishana kauli, na kwanza haijawahi kutokea katika historia ya chama chetu vikao vya kamati kuu kufanyika nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, ni uzushi huo," amesema Mrema.

No comments :
Post a Comment