Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 18, 2018

Chadema yawajibu wanaohoji matumizi ya Ruzuku? Kubenea, Komu kikaangoni!


Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeweka hadharani picha za magari yao mapya ambayo yatatumika katika shughuli za uenezi wa chama hicho ikiwa ni pamoja na kusaidia programu za uchaguzi na kueneza sera za chama zilizohuishwa na kuzinduliwa hivi karibuni.

Mkurugenzi wa Itifaki, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema amethibitisha uwepo wa gari hizo mpya.

Kwa siku za hivi karibuni wabunge na makada wa Chadema ambao wamekuwa wakikihama chama hicho wamekuwa wakihoji matumizi ya ruzuku ya chama hicho ambapo kwa mwezi wamekuwa wakipata Milioni 300, " Hapana siyo kwamba tumeonesha ili kuwajibu wanaohoji matumizi ya ruzuku, ni utaratibu tu wa Chama katika kuwaonesha wanachama na wafuasi wake mali za chama," imesema taarifa kutoka Chadema.

Kwa upande mwingine kamati kuu ya chama hicho imewahoji wabunge wake wawili wanaotuhumiwa kupanga njama za kukihujumu chama ambao ni Saed Kubenea wa jimbo la Ubungo na Anthony Komu wa Moshi Vijijini.

No comments :

Post a Comment