Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 16, 2018

Je, Upi ni Muda Sahihi wa Kufanya Mazoezi!


Ni ngumu sana kupata muda wa kufanya mazoezi kutokana na ratiba zetu kuwa ngumu, zimebana sana. Inaweza ikawa ni ngumu sana kubana ratiba zetu hata kama tunafahamu unyeti wa mazoezi katika afya zetu. Hata hivyo kwa kujua muda sahihi wa kwenda kufanya mazoezi ingetusaidia kufikia malengo yetu ya juu ya ubora kiafya.

Hebu tuone ni muda gani unafaa zaidi kwa mazoezi. Asubuhi, mchana au usiku?

Kufanya Mazoezi Asubuhi
Kiukweli kuna faida nyingi sana za kufanya mazoezi asubuhi. Kwanza kabisa, utakuwa umemalizana na suala la mazoezi hata kabla ya kuanza siku yako.

Inamaanisha utaanza siku yako na endofinsi -- furaha tele, na hisia nzuri za kujisikia kwamba umekamilisha wajibu kabla ya saa 3 asubuhi jambo ambalo wengine wanashindwa siku nzima. Na hii ni namna ya kuhamasisha furaha katika maisha yako.

Zaidi sana hutakuwa na wasiwasi wa kufanya mazoezi baadaye mchana au jioni. Hii itakuwa nafuu, na kukupatia muda wa kuandaa chakula cha usiku, kupiga stori na marafiki, na kukupatia pumziko safi.

Faida Kisayansi
Tafiti zinakubaliana na dhana ya kufanya mazoezi asubuhi. Matokeo ya utafiti  yaliyochapwa katika Medicine and science in sports and exercise kuchunguza namna wanawake walivyoitikia chakula baada ya kufanya mazoezi kitu cha kwanza asubuhi. Washiriki- wale wenye uzito wa kawaida wa mwili , na wenye kiriba tumbo- walitembea kwa haraka kwa dakika 45, walivutiwa kidogo sana na picha za vyakula vitamu zenye kuvutia ukilinganisha na wakati waliposhindwa kufanya mazoezi kabisa.

Katika siku ambazo washiriki walifanya mazoezi asubuhi, waliongeza uwezo wao wa kufanya kazi siku hiyo mara dufu ukilinganisha na siku ambazo hawakufanya mazoezi. Faida nyingine ya kufanya mazoezi asubuhi ni pamoja na kuongeza shughuli za kikemikali za mwili (metabolism), kwa maana ya kwamba utachoma nishati (calories) katika mwili wako siku nzima kadri unavyozitumia kuliko usiku wakati unapolala.

Sababu nyingine ya kufanya mazoezi asubuhi? Chunguzi zinaonesha kuwa kufanya mazoezi jioni kunaweza kuathiri usingizi wako. Mazoezi huongeza mapigo ya moyo na jotoridi. Inamaanisha vipindi vya kutoka jasho usiku inaweza kupaisha usingizi wako na kuharibu ubora wa usingizi wako. Chunguzi zinaonesha kwamba kufanya mazoezi saa 1 asubuhi, ukilinganisha na baadaye mchana au jioni, inaweza kuwasaidia watu kupata usingizi mtamu usiku.

Hoja moja zaidi kuhusu kufanya mazoezi asubuhi ni kwamba mazoezi wakati hujala chochote yanaweza kuchoma mafuta mwilini. Mazoezi yanachoma hadi 20% asilimia ya mafuta mwilini kama utayafanya asubuhi kabla ya kula chochote.

Kufanya Mazoezi Mchana au Usiku
Wakati bora zaidi kufanya mazoezi asubuhi, mazoezi mchana au baada ya masaa ya kazi nayo pia yamethibitishwa kuwa yana raha zake. Kupanga matembezi wakati wa jioni inamaanisha utapata usingizi zaidi asubuhi. Lakini kunafaida nyingine, pia!

Faida Kisayansi
Uchunguzi umegundua kwamba kilele cha uwezo wa mwili wako kufanya kazi hufikia wakati wa mchana. Jotoridi la mwili wako huongezeka mchana wote, kuweka sawa utendaji wa misuli na kuipa nguvu, kazi za vimengenya (enzymes), na uvumilivu katika kufanya kazi.

Kati ya saa 8 mchana na 12 jioni, jotoridi la mwili wako lipo juu zaidi. Hii inamaanisha utakapofanya mazoezi ni muda ambao mwili upo tayari zaidi, kufanya kuwa muda mzuri wa kufanya mazoezi.

Mchana na jioni, ndio muda ambao shughuli za kikemikali za mwili zipo juu sana, ambapo ni muhimu kwa mazoezi hasa yanayohusisha mafunzo ya mazoezi mazito.

Wakati baadhi wakitahadharisha namna ambavyo kufanya mazoezi usiku kunaweza kuhatarisha usingizi, uchunguzi mmoja uligundua kwamba wale waliofanya mazoezi ya kunyanyua uzani jioni walipata usingizi bora  na walilala kwa muda mrefu zaidi kuliko wale ambao walifanya hivyo hivyo asubuhi.

Maamuzi ya Mwisho
Kwa hiyo muda upi ndio ni bora zaidi? Wakati sayansi na chunguzi zikionekana kupingana, kitu kimoja kipo wazi: Kufanya mazoezi ni muhimu, haijalishi unafanya wakati gani.

Kitu cha msingi ni kwamba tafuta wakati katika siku inayokufaa wewe na ratiba zako fanya mazoezi na zingatia muda huo. Kwa kuzingatia ratiba ileile kila siku itakusaidia kujiapatia mafunzo ambayo yatakusaidia kupata faida kubwa zaidi.
/Benson Chonya

No comments :

Post a Comment